Jumuiya ya Qur'an na Sunnah ya Africa ya Mashariki [QSSEA]

WAKAAZI WA KISIMANI WANA SABABU YA KUTABASAMU

Mwezi mtukufu wa ramadhani umewadia na zawadi kubwa kwa wakaazi wa mtaa wa Kisimani kwa kuanzishwa Madrasa ya bure ya kuhifadhishwa watoto Kitabu cha Qur’an. Afueni hiyo imekuja katika wakati ambapo mapambano ya gharama za kimaisha na kusomesha mtoto imekuwa ni tatizo kubwa kwa wazazi. Madrasa hiyo imeanzishwa katika Masjid Sunnah hapo Kisimani kwa idadi ya wanafunzi 30 peke yake kutokana na nafasi ndogo ya Msikiti huo. Mradi wa kuanzishwa kwa Madrasa hiyo umedhaminiwa na michango ya wafadhili mbalimbali kwa kujitolea ili watoto wasikose ilimu yao ya dini kwa sababu ya ugumu wa maisha. Nafasi hizo za watoto kati ya miaka 7 hadi 15 zimewalenga familia ambazo zilizokuwa na hamu ya kusomesha watoto wao, hususan kuwahifadhisha Qur’an kwa moyo. Wazazi hao walojawa na furaha na kuona kama ni ndoto ya kusomeshewa watoto wao bila ya malipo. Imamu wa Masjid Sunnah, Bombolulu, amewahakikishia Waislamu kutoka sehemu yoyote yakwamba wanaruhusiwa kuleta watoto wao hapo Madrasa maadamu nafasi hazijajaa, na vilevile ameomba ushirikiano baina ya Masjid Sunnah na wazazi hao uendelee kudumishwa ili kupatikane natija kwa vizazi vyetu. Watenda kheri vilevile wamehimizwa kujiunga na wenzao katika kujitolea michango yao ili Madrasa iimarike katika siku za usoni.

MAKALA MAPYA

RIFQAN AHL AS-SUNNAH BI AHL AS-SUNNAH - SHEIKH ABDUL-MUHSIN AL- ABBÂD ‎‎(hafidhahullāh)‎
WASIFU WA SHEIKH ALI IBN HASAN IBN 'ABDULHAMID AL-HALABI - QSSEA‎
NASWAHA YA SHEIKH ABDUL-MUHSIN AL- ABBÂD KWA WANAFUNZI WA KI’ILIMU [TWALABATUL ‘ILM] - SHEIKH ABDUL-MUHSIN AL- ABBÂD ‎‎(hafidhahullāh)‎
NASWAHA YA SHEIKH ABDUL-MUHSIN AL- ABBÂD KWA SHEIKH RABI' BIN HADI AL-MADKHALI (حفظهما الله) - SHEIKH ABDUL-MUHSIN AL- ABBÂD ‎‎(hafidhahullāh)‎
‎TUNAMUHUKUMU VIPI MTU KUWA NI SALAFI AU SI SALAFI? Sheikh 'Abdul-Maalik ar-Ramadhaani ‎‎(hafidhahullāh)‎
MANHAJ YA ISIS - Sheikh Mash-hur Hasan Āl Salmân (hafidhahullâh)
NI NANI ALIYEMTANGULIA IMÂM AL-ALBÂNI KUHUSU MAKATAZO YA KUFUNGA SIKU YA JUMAMOSI - Sheikh Mash-hur Hasan Āl Salmân (hafidhahullâh)SOMA MAKALA ZAIDI...