
Ifuatayo ni tafsiri kutoka katika 'Fataawaa al-Albaanee (baadhi ya kandaa za tepu zilizonukuliwa za Shaykh) wakati shaykh alipoulizwa rai yake kuhusu Jihaad.
Bayana kwa mukhtasar:
Ndugu zangu wapendwa waume kwa wake ningelipenda kuidhihirisha bayana ya fatwa
ifuatayo ya Shaykh wetu mpendwa, Shaykh Muhammad Naasir ud-Deen Al-Albaani
(rahimahullaah)...
Asli yake ilipatikana kutoka katika kanda ya tepu ya darasa ya Shaykh
Al-Albaani, ambamo ndani yake aliulizwa suali kuhusiana na matayarisho ya
kujiandaa kwa Jihaad ya kufanya mashambulizi; ambapo Waislamu wanapotakiwa
kutoka katika miji yao ya kiislamu ili kupigana vita na Makuffaar, kinyume cha
Jihaad ya ki-leo ya kujihami; ambapo miji ya kiislamu imevamiwa na kushambuliwa
na Makuffaar, kwenye hali zote hizo - kama alivyoeleza waziwazi Shaykh - vita
hivyo vyao vinakuwa ni Fard 'ayn juu ya Waislamu (yaani: waajib unaompasa kila
mwenye uwezo).
Inaonekana yakwamba kiini cha suala hilo, au malengo ya mjadala kuhusu Fatwa
hii - ambao ungelikuwa ni wenye kuondoa shaka katika suala hili - kwa sababu
fulani ukawachwa bila ya mazingatio yoyote...
Na kwa hakika, matokeo ya kutoelewa vyema, au kufahamu vibaya huko kwa ajili
ya ukosefu huu ni bahati mbaya... Kwa sababu Fatwa hii imetapakaa katika
mitandao, na kawaida hufuatana na madai ya urongo yasemayo eti uimarishaji wa
Jihaad siku hizi na zama hizi zetu - iwapo ni wa Kuvamia, au Kujihami - haijuzu
pasi na kuwepo Khaleefah, au Imaam kwa Waislamu wote.
Lakini madai haya ni ya uwongo, na upuzi. Kwani yoyote mwenye kufanya utafiti
wa zama za kina Tatar (kina Mongol) - ambao waliotangazwa kuwa ni Makuffaar na
Ma 'Ulamaa - Waliiuwa Khilaafah ya Waislamu, kisha wakajichagulia wenyewe
utawala wa Ulimwengu wa Kiislamu, mtu atajionea, bi-idhnillaah, yakwamba -
hatakama hapakuwepo na Khilaafah - Waislamu wakaingia vitani na kupigana Jihaad,
wakawauwa na kuwatenza nguvu Makuffaar, hivyobasi kui-imarisha tena
Khilaafah kwa mara nyengine tena - na miongoni mwao akiwemo Ibn Taymiyyah
(rahimahullaah) mwenyewe!
Kwahivyo, haya madai ya kuhusu Jihaad ya kujihami, ni ya urongo.
Vilevile inajulikana, kama ilivyoelezwa katika Fatwa hii, yakwamba Shaykh
Al-Albaani Allaah (Ta'aala) Alija'alie kaburi lake ling'are) anaamini yakwamba
Jihaad ya huko Afghanistan ilikuwa ni Jihaad iliyosihi - na pia, ni jambo la
dhahiri, hapakuwepo Khilaafah, au Ameer kwa Waislamu wote waliokuweko wakati
huwo... sasa hali hii ya urongo ilitoka wapi?... Haikutoka kwa Ma'ulamaa wa
kikweli.
Mtu akiwa na ikhlasi katika kuutafuta ukweli wa mas-ala haya, basi namnasihi
kila mmoja ajipatie baadhi ya darsa za Shaykh Al-Albaani kuhusu Jihaad, ambapo
ameeleza msimamo wake waziwazi kuhusu aina mbili za Jihaad - Jihaad ya Uvamizi
na Jihaad ya Kujihami.
Kwa mfano, katika kanda yake ya tepu "Fataawa hawl al-Jihaad
al-afghaani."[1] mwanafunzi mmoja
alimuuliza iwapo Jihaad ya Afghanistan ni Fard 'ayn, au Fard kifaayah, na Shaykh
akajibu yakwamba ni Fard 'ayn, kwa sababu idadi ya Waislamu wanaopigana na jeshi
la Mushrikeen la Urusi (Russia) halikuwa la kutosha. Pia akasema yakwamba kila
Muislamu ilimpasa ashiriki kwenye Jihaad hii...
: Waislamu wanapigana kwa ajili ya kulienua neno la Allaah (Ta'aala), na/au
kuzilinda ardhi zao Kuhusu suala la Jihaad ya Uvamizi (ambayo inayofuata), basi
namnasihi kila mmoja aisikilize tepu ya Shaykh, "Shubuhaat mud'iyee
al-Jihaad." Katika darsa hii akaubainisha msimamo wake kuhusu kujiandaa kwa
Jihaad ya Uvamizi, na ni aina hii ya Jihaad ambayo - kulingana na maoni ya
Shaykh - inaweza kutekelezwa chini ya Ukhalifa, na hii Jihaad ya Kujihami
(yaanikutoka kwa Makuffaar) inaweza kutekelezwa chini ya Ameer, au bila ya
Ameer wa Waislamu wote...
Na hii ndiyo misemo ya Ma'ulamaa.
Na asili ya kila uongofu unatoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aala).
Abu Suhayb
Jawabu:
"Kuhusu Jihaad, Ewe ndugu yangu, katika wakati huu na kabla ya wakati huu,
ni fard 'ayn, kwa sababu matatizo tuliyo nayo si matatizo ya Bosnia na Chechnya
(peke yao) amabyo yamewaathiri vijana wengi na kuwatia hamasa. Kwani hapa
jiranini mwetu, kuna Mayahudi ambao walioivamia Falesteen, na hata nchi moja ya
Kiislamu haijajisongeza kutekeleza wajibu wa kupambana nao Jihaad, na kuwang'oa
na kuwatumbukiza baharini, kama walivyosema baadhi au mmoja wa Ma-Rais wa
nchi za Kiislamu.
Na nukta iliyoko hapa ni kwamba Jihaad ni fard ayn, kwa sababu nchi nyingi za
Kiislamu zilivamiwa zamani mpaka hivi sasa na Makuffaar. Na mifano ya Uvamizi
huwo haikufichika kwa Muislamu mwenye kujishughulisha na harakati za waislamu,
bila ya kuvitaja vikundi vya Kiislamu au vipote vya Kiislamu au nchi za
Kiislamu.
Lakini Jihaad ina nguzo na sheria zake, na sisi - kikundi cha wanavyuoni wa
Kiislamu - tunaamini yakwamba Jihaad ya faradhi itawalazimu peke yake waislamu
ambao watakaosaidiana katika kusimamisha yale yaliyoamrishwa juu yao kutoka
katika Jihaad dhidi ya makuffaar, na kuwang'oa kutoka katika ardhi au nchi
walizozivamia.
Na kwa sasa hatuhitaji kuleta ushahidi kutoka katika Kitaab na Sunnah, kwani
nukta hii imeafikiwa na wanavyuoni wote - yakwamba Jihaad ni fard ayn
ikiwa sehemu ya ardhi ya waislamu imevamiwa, sasa itakuwaje iwapo uvamizi huwo
umetokea kwenye ardhi nyingi.?!
Lakini, kwa bahati mbaya napenda kusema yakwamba Jihaad hii ambayo ni fard -
bali ni fard ayn - si kitu kinachowezekana kutekelezwa na watu binafsi kama
ilivyokuja kwenye suali lenyewe, bali hata na baadhi ya makundi ya kiislamu. Kwa
sababu mifano ya Jihaad kama hii, haswa katika hizi zama zetu ambazo uwezo wa
ki-vita umekuwa mwingi, haiwezekani kutekelezwa na vikundi vya kiislamu na
watu binasfi ndio hata usiwataje! Lakini wajibu ni juu ya hizi Serikali, na zile
nchi za kiislamu ambazo zilizo na uwezo wa kujitayarisha kwa vita, na, na
uwezo wa vita vya kisasa, ambao watakaposhirikiana kwa ikhlaas kwa Jihaad hii,
basi watakuwa ni wenye kuitekeleza fard ayn. Lakini, kwa masikitiko makubwa,
nchi hizi hata hazijatukusa viungo vyao katika kulitekeleza jambo hilo.
Kwahivyo, pengine wanalihusisha suala hilo la Jihaad na makundi na mapote
mbalimbali ya Uislamu, ambapo haya hayana uwezo wowote wa kuzuiya kuingiliwa
/uvamizi wa Makuffaar. Na matukio ya kilimwengu yameshuhudilia uhakika yakwamba
kila kikundi cha Kiislamu kinachojaribu, emma kupambana na adui kwa mfano kama
ilivyotokea huko Afghanistan, au kwa kufanya uasi dhidi ya kiongozi ambae
Ukafiri wake umedhihiri, kwa mfano, kama huko Algeria - kisha matukio haya ya
bahati mbaya yanaonyesha kuwa Jihaad ya watu binafsi au Jihaad ya kikundi
haileti matunda yanayotarajiwa, nalo ni kwamba Neno la Allaah lifanywe kuwa bora
kuliko chochote.
Sasa kwahivyo, tunaamini yakwamba Jihaad hii haiwezekani isipokuwa kwanza iwe
chini ya mamlaka ya Kiislamu, na chini ya kikundi cha Kiislamu chenye watu
kutoka katika nchi mbalimbali, badala ya wote kutoka katika nchi moja au sehemu
moja.
Na juu ya hayo kupatikane umuhimu wa Taqwaa ya Allaah, kwa kujiepusha na yale
ambayo Allaah aliyoyaharamisha kutoka katika mambo ya kawaida yanayojulikana
sana miongoni mwa Waislamu, lakini kwa masikitiko makubwa wao wako mbali sana na
kuyatekeleza hayo.
Na pia tumetaja - na najaribu kuyafupisha maneno yangu kadiri ya uwezekano
uliopo - mara nyingi yale yanayowasibu waislamu leo, huu utwevu na
udhalilifu/fedheha mambo ambayo hayakuwa ni yenye kujulikana kabisa katika
tareekh (historia) ya Kiislamu, ni kwamba Waislamu hawakuweza kutekeleza, kwa
uchache, hata aya moja ya Qur'aan... na hayo ni maneno ya Allaah (kama
yalivyofasiriwa):
"Enyi mlioamini! Mkiinusuru dini ya Allaah, naye Atakunusuruni na
Ataithubutisha miguu yenu". [Soorah Muhammad 47:7]
Hapana shaka yoyote yakwamba nusra hii ya waislamu kutoka kwa Allaah, ni
nusra ya kuibainisha Hukmu ya ki-Sheriya ikawa ni ukweli wenye kutekelezwa, na
kwa bahati mbaya jambo hili halizingatiwi katika nchi nyingi za Kiislamu, au
hata kwa waislamu wenyewe nafsi zao. Na miongoni mwa hizo nchi za Kiislamu zenye
baadhi ya chembe-chembe za hukmu kulingana na Sheriya ya Allaah hazijaweza,
mpaka sasa kupiga mbiu ya mwito wa Jihaad.
Na kutokana na hayo waislamu na mataifa watabakia dhaifu maadamu haijatokea
nchi yoyote ya kiislamu iliyoienua bendera ya Jihaad, na Jihaad hiyo
ambayo inayoitisha mapambano dhidi ya wale walio karibu nao, sio wale walio
katika upeo wa mbali na wao. Kwa waislamu, pamoja na nchi zao, na makundi yao,
na vipote, na kwa watu binafsi, iwapo hawatoweza kupigana Jihaad na wale
waliopakana nao au walio karibu nao basi hawatoweza kupigana Jihaad na wale
walio mbali nao... kwa mfano Eritrea, Somalia, Bosnia na Chechnya.
Sasa tutayataja kutokana na haya, majukumu juu ya vijana wa Kiislamu kila
mmoja kwa nafsi yake na kwa makundi na kwa mapote yakwamba kwanza wausambaze
ujumbe wa Uislamu kwenye nchi, na pili ni kwa viongozi - na ufahamu huwo (wa
kisawasawa) uambatane na watu wote hao wahukumiane kulingana na yale
yaliyoteremshwa na Allaah.
Kiongozi anatakiwa atawale kulingana na yale yaliyoteremshwa na kuamrishwa
katika Kitabu cha Allaah. Na kila mtu kwa nafsi yake ahukumu kulingana na yale
yaliyoteremshwa na kuamrishwa katika Kitabu cha Allaah... Najua mimi leo vijana
wengi, na makundi na mapote, huwasukumizia majukumu hayo (mambo ya kilimwengu)
viongozi peke yao, haliyakuwa imethubutu katika imani yangu yakwamba majukumu ni
yenye kumkabili kila mtu, makundi na mapote, kama yanavyowakabili viongozi hawa!
Hii ni kwa sababu serikali hizi zimesimamishwa kutoka katika ardhi za
waislamu...waislamu hawa ambao waliolinganiwa kwa hadeeth mbili kutoka kwa Mtume
(Sallallaahu 'alayhi wasallam)... ya kwanza ni maneno yake (Sallallaahu
'alayhi wasallam) aliposema:
'Mutakapo jishughulisha na biashara za riba na kushikamana na mikiya ya
ng'ombe, na mukaridhika na mambo ya ukulima (mashamba) na mukawachana na
kupigana jihaad kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wata'aalah),
basi Mwenyezi Mungu atawadhalilisha. Na hatowaondolea udhalilifu huo mpaka
muregee kwenye dini yenu'".
Na hadeeth nyengine ni maneno yake (Sallallaahu 'alayhi wasallam)
aliposema:
"Hivi karibuni mataifa yataitana kuungana dhidi yenu, kama vile watu
wanavyoitana kuja kula kutoka kwenye sinia ya chakula."
Akauliza mtu mmoja: "Litakuwa jambo hilo kwa ajili ya idadi yetu
itakavyokuwa chache, Ewe Rasoolullaah (Sallallaahu 'alayhi wasallam)?"
Akajibu Mtume (Sallallaahu 'alayhi wasallam): "Laa, mutakuwa
idadi yenu ni kubwa, lakini mutakuwa ghuthaa'a kama zile takataka za povu
zinazo-olea juu ya kidimbwi cha maji, na Allaah (Subhaanahu wata'aalah) ataondoa
khofu kutoka katika nyoyo za maadui zenu (ya kuwaogopa nyinyi) na atawaekea
kwenye nyoyo zenu WAHN."
Wale waliokuwepo pale wakauliza: "Na ni nini hiyo WAHN, ewe Rasoolullaah (Sallallaahu
'alayhi wasallam)?"
Akajibu Mtume (Sallallaahu 'alayhi wasallam): "Ni kuyapenda
maisha ya kidunia na kuyachukia mauti.
Na matukioa kama haya yaliyotajwa na Mtume (Sallallaahu 'alayhi wasallam)
katika hadeeth hii sasa yametokea katika jamii zote za waislamu, na ni miongoni
mwa dhulma zilizodhahiri zenye kuupalilia ukandamizaji huu kwa
waislamu mpaka nyoyo za viongozi, na watu binafsi zikafunikwa zote na weusi
(kutokana na madhambi yao).
Miji ya Kiislamu haihukumiani kwa yale yaliyoteremshwa na Allaah, na lau kama
kuna mji mmoja miongoni mwao ambao (unaodai) kuhukumu kwa yale yaliyoteremshwa
na Allaah, basi ishara ya kwanza iliyo wazi yenye kuonyesha yakwamba
haihukumiani kwa yale yaliyoteremshwa na Allaah ni kwamba hawaupaazi mwito wa
Jihaad.
Sasa ikiwa wakati huu sio wakati ambao Jihaad katika njia ya Allaah
haiwezekani kuwa waajib, na miji mengi ya kiislamu imeshavamiwa, basi ni lini
hapo Jihaad itakapokuwa wajibu?
Lakini tatizo ni kwamba - na huu ndio moyo wa suala zima - ni kwamba hakuna
yoyote miongoni mwetu mwenye uwezo wa kuiendeleza (Jihaad hii), kwanini?... Kwa
sababu sisi twazama ndani ya madhambi, na twazama ndani ya ikhtilafu za vipote
na ikhtilafu za kitaifa , na sisi twajua yakwamba mlango mmoja unaoelekeza
kwenye udhaifu na kushindwa ni kukhitalifiana miongoni mwa waislamu wenyewe.
Na hivi karibuni tulifikwa na mtihani wenye kusikitisha sana, nao ni Jihaad
ya Afghani, ambapo tulikuwa tukitarajia yakwamba hatima yake itakuwa ni ushindi
kwa waislamu, na kukawa na alama madhubuti za kupanda mbegu ya Taifa la
Kiislamu. Kisha mwishoe na matokeo yake yakageuka na kuwa kinyume kabisa (cha
vile kulivyotarajiwa) kutokana na alama za ushindi wa mapema juu ya adui, wa-communisti
(shuyuiyyeen), walififia wakati tafauti baina ya makabila zikawafanya
wagawanyike kwa makundi saba, na Uislamu wao walioufanya kuwa ndiyo Deen
haukuwazuiya kufanya hivyo, na Mola wetu akasema (kama ilivyofasiriwa):
"...wala msiwe katika washirikina. Katika wale walioitenga dini yao
na wakawa makundi makundi; kila kikundi kinamfurahia kilicho nacho."
[Soorah Ar-Rum 30:31-32]
Kwahivyo, ni juu ya yule mwenye kupenda kuhudhuria Jihaad ajiandae vilivyo
kwa Jihaad, na maandalizi ya kupata ushindi, na kwa bahati mbaya jambo hilo
halizingatiwi katika zama zetu hizi. Na Allaah (Subhaanahu wata'aalah)
Amesema katika Qur'aan Tukufu, (kama ilivyofasiriwa):
"Hakika Mwenyezi Mungu habadili yaliyoko kwa watu mpaka wabadili wao
yaliyomo katika nafsi zao." [Soorah Ar-Ra'd 13:11]
Kwahivyo, tunamtaka kila muislamu, kila kikundi na kila kipote,
wasizizungumze Serikali zenye kujishughulisha kuusambaza Uislamu uliotahirika na
ulio saheeh, uliotahirika kutokana na kila jambo la urongo lililoingizwa ndani
yake kwenye zama tafauti, na kisha kuwalea Waislamu juu ya Uislamu huu ulio
safi.
Siku ambayo alama hizi zitakapoanza, na zikawa zadhihirika katika ardhi hii
pana ya Kiislamu, basi siku hiyo ndiyo zile alama za kuwa tayari kuithibitisha
Jihaad ya Fard ayn itakapoanza. Hawa watu wenye kutaharuki wanaokwenda katika
nchi nyingi za Kiislamu zilizovamiwa/zilizoshambuliwa na Makuffaar kama vile
Bosnia na Chechnya kwa mfano... ni silaha gani walizonazo wao? ni kina nani
viongozi ambao wenye uwezo wa kuwasimamia na kuwaongoza na kuwapa maamrisho ya
kupigana chini ya mamlaka na chini ya bendera moja? Kwahivyo kama
kungelipatikana mamlaka ya aina moja peke yake basi tungeliyaona (matunda) ya
Jihaad kama tulivyoyaona huko Afghanistan (yaani: ushindi juu ya adui).
Kwahivyo, Allaah (Subhaanahu wata'aalah) Amesema katika Qur'aan Tukufu,
(kama ilivyofasiriwa):
"Basi waandalieni nguvu mziwezao, na mafarasi yaliyofungwa,
tayari tayari, ili kwazo (nguvu hizi) muogopeshe maadui wa Mwenyezi Mungu na
maadui zenu." [Soorah al-Anfaal, Aayah 8:60]
Yako wapi matayarisho hayo?! Na ni yupi mwenye uwezo wa matayarisho hayo?
Kila mtu kipekee?! Laa, Ni Serikali?...naam ni Serikali, na tunaweza sisi kusema
yakwamba michango yao ya matayarisho hayo si midogo...lakini matayarisho haya
yamepatikana kutoka kwa maadui zao... sasa ikisimama Jihaad baina ya Waislamu na
Ma-kuffaar, mara tu hawa waislamu hawatokuwa na uwezo wa kuwafikishia mahitaji
ya silaha majeshi yao isipokuwa kwa kununua kutoka kwa maadui zao.
Sasa kwaweza kupatikana ushindi na Jihaad kwa kununua silaha kutoka kwa
maadui wa waislamu?!
Haiwezekani namna hii, na kwa ajili hiyo, matayarisho haya yanatuamrisha
sisi, hayawezi kuimarishwa hata na nchi za Kiislamu, kwa sababu nchi za Kiislamu
zenyewe hununua silaha zao za maangamizi kutoka kwa maadui zao na mataifa yenye
ukandamizaji. Na kuna njia ya kuzitia ganzi silaha hizi (zisiweze kutumika)
wakati wao (waislamu) watakapodhamiria kuzitumia dhidi ya jeshi la makafiri. Na
kwa ajili hii, mimi nasema, na namalizia maneno yangu na jawabu langu kwa suala
hili yakwamba pindi Allaah Aliposema (kama ilivyofasiriwa):
"Basi waandalieni nguvu mziwezao..."
Tangazo hili lilikuwa ni kwa Maswahaba wa Mtume (Sallallaahu 'alayhi
wasallam), kisha tangazo hilo likawa ni kwa mujtama' mzima wa waislamu kwa
kutokana na ujumla wa maandishi yenyewe. Lakini tangazo hili liliwaelekea
Maswahaba baada yakwamba wamelelewa juu ya malezi ya Uislamu saheeh mpaka wakawa
na uwezo wa kuimarisha mfano wa tangazo hilo - kutayarisha nguvu za kilimwengu
baada ya kutayarisha nguvu za kiroho ndani ya nafsi zao au baina yao wenyewe,
kutokana na malezi waliyokulia nayo kutoka kwa Mtume wao (Sallallaahu 'alayhi
wasallam).
Na taarekh (historia) hujirudia yenyewe...Sasa inatakikaniwa kupatikane
malezi ya taifa kutoka katika Mataifa ya Kiislamu ili kuwe na uwezekano wa taifa
hilo kuimarisha haya mambo ya matayarisho ya kilimwengu, na sisi leo hatuoni
taifa lililoimarisha wajibu huu ambao tunaweza kuufafanua kwa maneno mawili:
tasfiyyah na tarbiyyah.
(Bali) twajiona kama watu walio tapakaa kila mmoja na nafsi yake. Na lau kama
pangelikuwa na kikundi, na juu ya kikundi hichi kuwe na kiongozi mwenye
kufanyiwa utiifu na waislamu wote, na akainyanyua bendera ya Jihaad dhidi ya
maadui: Jambo hili bado halijawahi kutokea, na kwa ajili hii tunaitisha kuwepo
kwa utangulizi/matayarisho ya hii Jihaad Tukufu.
Amma kuhusu kuwa na pupa (kwa hawa watu) na hamasa ingawaje hata hiyo Jihaad
ya nafsi haijaonekana kwao - na huwo ndiwo ufahamu saheeh wa Kiislamu, na
kuutekeleza kwa ushirikiano, na kwamba aweko juu yao kiongozi baada ya hayo,
ambae atakaewahimiza wajiandae kwa nguvu waziwezao na silaha: Kwahivyo siku
tutakapo-ona mambo mfano wa hayo, siku hiyo waislamu watakuwa ni wenye
kuushangilia ushindi wa Allaah, na Allaah humsaidia amtakae. Hili ndilo jawabu
langu la suali lako."
Nukta ya maelezo:
|