Walivyosema Wanavyuoni Kuhusu Jamaa'at ut-Tableegh
Imetayarishwa Na: Sheikh Rabee' bin Haadee al-Madkhalee
Imefasiriwa Na: Abu Farida Muhammad A Basawad.

Bismillaahir Rahmaanir Raheem


Sifa zote njema ni zenye kumthubutukia Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wata'aalah) Peke Yake, na swala na salamu zimfikie mjumbe Wake (Sallallahu 'alyhi wasallam), ahli zake na maswahaba zake na wote wale waloufuata uongofu wake. Ama kwa yafuatayo, mwanzo kabisa: Kuna kurasa fulani zilizonifikia mimi ambazo zina taarifa kutoka kwa ma-'Al-laamah wa ki-Salafi wawili, Sheikh Ibn Baaz na Sheikh Ibn al-'Uthaymeen ambazo zinasambazwa na Jamaa'at ut-Tableegh miongoni mwa wajinga na wale wasojua ukweli wa Manhaj na 'Aqeedah zao mbovu. Na ukweli ni kwamba taarifa hizo za wanavyuoni hao wawili zinawaunga wao mkono.

Kwahivyo taarifa kutoka kwa Sheikh Ibn Baaz ime-egemezwa juu ya maelezo kutoka kwa mfuasi wa Tableeghee, au mtu mwenye kuwapendelea wao, yaliosimuliwa kwa Sheikh Ibn Baaz, kinyume na vile misimamo yao ilivyo na kutoa ufafanuzi ulio kinyume na ukweli wa hali yao na kukubaliana na yale tusemayo ya taarifa ya Sheikh Ibn Baaz (Rahimahullaah): "... na hapana shaka yoyote, kwa hakika watu wako katika hali ya kuhitaji zaidi mikutano mizuri kama hii inayokusanya watu juu ya makumbusho ya Mwenyezi Mungu na kuwaita kwenye kushirikiana katika Uislamu na kutekeleza mafundisho yake na kuondolea mbali mambo ya uzushi na ushirikina kutoka katika Tawheed (ya Mwenyezi Mungu) ..." [Tizama fatwa yake, Nambari ya kumbukumbu 1007, mnamo 17/08/1407 A.H ambayo inayosambazwa na Jamaa'at ut-Tableegh sasa]

Utaona (fatwa) hii yaonyesha msimulizi akitaja kwenye maelezo yake yakwamba kwa hakika jamaa'ah hii yaitisha kwenye kushikamana na Uislamu, kutekeleza mafundisho yake na kuitakasa Tawheed (ya Mwenyezi Mungu) na uzushi (wote) na ushirikina. Na kama ilivyo matokeo yake, Sheikh akawasifu. Na lau kama msimulizi huyu wa maelezo angesema ukweli na kuwafafanua wao juu ya uhakika wao na akaeleza ukweli wa manhaj yao potofu, basi hatungeliona kutoka kwa Imaam Ibn Baaz, Salafee, alie mpwekeshaji, isipokuwa kuwakanusha na kuwatahadharisha watu dhidi yao na uzushi wao, kama alivyokwisha fanya kwenye fatwa yake ya mwisho kuwahusu wao iliyoambatana na hii (hapo juu). Na katika taarifa ya 'Al-laamah Ibn al-'Uthaymeen kuhusiana na kile kinachowaunga mkono, tizama hii taarifa yake kama ifuatavyo: "Angalia: Iwapo ikhtilafu (ya maoni) ipo kwenye mas-ala ya 'aqeedah, basi inawajibika kurekebisha (jambo hili) na pia lolote lenye kwenda kinyume na njia ya Salaf. Kwa hakika, ni wajibu kuchukia jambo hilo na kuwaonya wenye kushikamana na (njia ya wale) jambo lenye kwenda kinyume na njia ya salaf katika hali hii.
[Tizama fatawaa Ibn al-'Uthaymeen- Volume 2, Ukurasa 939-944 iliyofanana na ile inayosambazwa na Jamaa'at ut-Tableegh].

Bila ya shaka, ikhtilafu ya maoni miongoni mwa salafi, Ahlus-Sunnah wat-Tawheed na Jamaa'at ut-Tableegh ni ikhtilafu kubwa mno zilizozama kwenye 'aqeedah na manhaj. Wao ni wafuasi wa njia ya Maatureediyyah ambao ndio waliozua katika sifa za Mwenyezi Mungu na ambao wametokamana na Soofiyyah katika 'Ibaadah zao na desturi, wenye kutoa bay'ah. Na kutokana na hayo, hao ndio wenye kuamini al-Hulool na wahdatil-wujood na kufanya ushirikina wa makaburi na mengine yasokuwa hayo katika upotofu (wao). Hapana shaka yoyote, Sheikh Ibn al-'Uthaymeen hajui hayo, na lau angeliyajua hayo kuwahusu wao, basi kwa hakika angeliwakanusha kwa upotofu wao (waloshikamana nao) na angelitoa onyo kali dhidi yao. Kwa hakika angeliwaburuta kwenye njia ya salafi, kama walivyofanya mashekhe wake wawili, Imaam Muhammad Ibn Ibraaheem na Imaam Ibn Baaz. Na kama vile walivyofanya kina Sheikh al-Albaani, Sheikh 'Abdur-Razzaak 'Afeefee, Sheikh Fawzaan, Sheikh Hamood at-Tuwayjaree, Sheikh Taqee ad-Deen al-Hilaalee, Sheikh Sa'd al-Hussayn, Sheikh Seif ar-Rahmaan, na Sheikh Muhammad Aslam. Katika makala yao, waliubainisha upotofu wa Jamaa'at ut-Tableegh na hatari zao na yale waliyoshikamana nayo kuhusiana na 'aqeedah na manhaj zao potofu. Ni bora kwa wanafunzi wenye bidii na wasio na machezo kuyapitia makala hayo.

Sheikh 'Abdur-Rahmaan al-Misree alirudi (kwenye hali yake ya kwanza) baada ya kuandika na kuwasifu Jamaa'at ut-Tableegh na akakiri makosa yake kwangu. Ama kuhusu Yoosuf al-Malaahee, yeye ni miongoni mwa wale waliokuwa nao kwa miaka mingi, kisha akawakanusha na kueleza 'aqeedah zao mbovu zilizopotoka, kisha kwa masikitiko akarudi tena kutoka kwenye uongofu na akaandika kitabu chengine kuwahusu wao. Kitabu chake cha mwanzo kilimsaidia pamoja na yale yalioandikwa na wanavyuoni wa manhaj kuwahusu wao na baadae kumkanusha yeye na upotofu wake. Kwahivyo, kulingana na hukmu ya Ilimu ya Jarh wat-Ta'deel, al-Jarh daima ni yenye kuitangulia at-Ta'deel. Sifa za aina yoyote za mtu hufutiliwa mbali, hata kama Tableegh ni wenye kufuata mfumo ulio saheeh wa hukmu za Kiislamu na kuandama njia ya wenye ilimu na kutoa nasiha za Uislamu na kwa Waislamu.
Imeandikwa na Sheikh Rabee' bin Haadee al-Madkhalee / 29 Muharram-1421 A.H

Fatwa ya Imaam 'Abdul-Aziz bin Baaz