
Fatwa ya mwisho ya Sheikh 'Abdul-'Azeez bin Baaz:
Onyo dhidi ya Jamaa'at ut-Tableegh:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu.
Muheshimiwa, Sheikh 'Abdul-'Azeez bin Baaz(Rahimahullaah) aliulizwa kuhusu Jamaa'at ut-Tableegh, kwahivyo mwenye suali akauliza:
Muheshimiwa Sheikh, sisi tunasikia kuhusu Jamaa'at ut-Tableegh na athari za Da'wah yao. Jee, ungelininasihi mimi nijiunge na jama'ah hii? Nataraji uongofu na nasiha kutoka kwako na Mwenyezi Mungu Akujazi kila la kheri.
Sheikh nae akamjibu kwa kusema:
Yeyote mwenye kuita watu kwenye (njia ya) Mwenyezi Mungu, basi huyo ni muballigh (mwenye kuufikiliza ujumbe (wa Uislamu)), kama ilivyotajwa kwenye hadeeth isemayo:
"Fikisheni kutoka kwangu, hata kama ni Aayah moja"
Hawa Jamaa'at ut-Tableegh wenye asili ya kutoka India wana upotofu mwingi sana. Wana namna nyingi sana za bid'ah na Shirk, kwahivyo hairuhusiwi kutoka nao, isipokuwa kwa yule mwenye ilimu ili atokapo nao asiwaridhie yale wafanyayo na awafunze hakki. Ama kuhusu kutoka nao na kushirikiana na kusaidiana nao, basi Laa!
Hayo ni kwa sababu wao wana upotofu, makosa na uchache wa ilimu. Hata hivyo ikiwa kuna watu wanaofanya tableegh wasiokuwa wao kutoka kwa wenye ilimu, basi hao inaruhusiwa kutoka nao kwa ajili ya da'wah.
Ikiwa palikuwa na mtu mwenye ilimu mwenye kutoka nao ili awaerevushe na kuwaongoza, pamoja na kuwafunza ili waache upotofu wao na kuandama njia ya Ahlus-Sunnah wal Jamaa'ah, (basi hilo ni jambo zuri).
[Kwahivyo, hawa Jamaa'at ut-Tableegh na wale wenye kuwahurumia, watanufaika na fatwa hii yenye kueleza ukweli wa 'aqeedah na manhaj zao na maandishi ya wanavyuoni wao ambao huwafuata ki-upofu].
Haya ni maneno yalionukuliwa kutoka kwenye kanda ya tepu: 'Fatwa Samaahatush-Sheikh 'Abdul-'Azeez bin Baaz kuhusu Jamaa'at ut-Tableegh iliyotolewa mjini Taif takriban miaka miwili kabla ya kifo cha Sheikh. Kanda hizo zinakanusha na kufichua siri za Jamaa'at ut-Tableegh na ile taarifa yake ya zamani kuwahusu wao iliyochapishwa kabla ya ukweli wao na manhaj zilipobainishwa kwake.]
Jamaa'at ut-Tableegh na Ikhwaan ni miongoni mwa mapote 72
Muheshimiwa, Sheikh 'Abdul-'Azeez bin Baaz(Rahimahullaah) aliulizwa:
Suali: "Mwenyezi Mungu(Subhaanahu wata'aalah) Akuja'alie kila la kheri (katika ne'ema zake). Katika hadeeth ya Mtume Muhammad(Sallallahu 'alayhi wasallam), kuhusiana na kugawanyika kwa Ummah, amesema:
'... na Ummah wangu utagawanyika vipote 72...'
Jee Sheikh, hawa Jamaa'at ut-Tableegh na yale walonayo, yakiwemo Shirk na mambo ya uzushi; na vilevile Jamaa'ah al-Ikhwaan al-Muslimeen, na yale walonayo yakiwemo mambo ya Hizbiyyah na ku'asi/ kufanya michafuko dhidi ya viongozi na ukosefu wa twa'a; Hawa ni miongoni mwa hayo mapote 72?"
Jawabu: "Wao ni miongoni mwa vipote 72. Yeyote mwenye kwenda kinyume na 'aqeedah ya Ahlus-Sunnah anaingia kwenye mkunjo huo wa vipote 72. Maana ya maneno ya Mtume(Sallallahu 'alayhi wasallam)'UMMAH WANGU' ni: Ummah wa Ijaabah- yaani Ummah wa kuitika: wale wenye kuitika mwito wa Mtume(Sallallahu 'alayhi wasallam) na wakambai'i yeye. Na maana ya vipote 73 ni kile kipote kitakacho shikamana na yeye na wakasimama wima katika dini yao na 72 ya vipote hivyo- wakiwemo miongoni mwao kuffaar, wafanyao ma'asia na wazushi wa kila aina". Akauliza tena mwenye Suali: "Jee mapote haya mawili (Jamaa'at ut-Tableegh na Jamaa'ah al-Ikhwaan al-Muslimeen) ni miongoni mwa hayo mapote 72?"
Akajibu: "Na'am, wao ni miongoni mwa mapote 72, pamoja na Murji'ah na wengine wasokuwa hao; Murji'ah na Khawaarij- Baadhi ya wanavyuoni wanawaona hawa Khawaarij kuwa ni miongoni mwa Kuffaar, walio nje ya mkunjo wa Uislamu hata kama wamo miongoni mwa mapote 72".
[Yamenukuliwa kutoka kwenye kanda za tepu za Sheikh- Darasa za Sharh-muntaqaa, mjini Taaif, takriban miaka miwili au michache kabla ya kufa kwake].
Kutoka na Kutembea nao - Sh. bin Baaz (Endelea)
|