Walivyosema Wanavyuoni Kuhusu Jamaa'at ut-Tableegh
Imetayarishwa Na: Sheikh Rabee' bin Haadee al-Madkhalee
Imefasiriwa Na: Abu Farida Muhammad A Basawad.

Bismillaahir Rahmaanir Raheem

Hukmu kuhusiana na kutoka / kutembea na Jamaa'at ut-Tableegh.

Muheshimiwa, Sheikh 'Abdul-'Azeez bin Baaz(Rahimahullaah)aliulizwa: Suali:"Mimi niliwahi kusafiri na Jamaa'at ut-Tableegh na kuelekea miji ya India na Pakistan. Tulikuwa tukijumuika na kuswali katika Misikiti yenye makaburi ndani yake, na niliwahi kusikia yakwamba swala kwenye msikiti wenye kaburi haifai. Ni nini rai yako kuhusu swala zangu, nizirudie tena? Na ni nini hukmu ya kuandamana nao kwenye sehemu hizi?"

Jawabu: "Kwa hakika Jamaa'at ut-Tableegh hawana ilimu iliyo saheeh kuhusiana na mas-ala ya 'aqeedah, kwahivyo hairuhusiwi kutembea nao isipokuwa kwa yule mwenye ilimu ya kweli ya 'aqeedah saheeh ya Ahlus-Sunnah wal-Jamaa'ah. Katika hali hii, anaweza kuwazindua, kuwapa nasiha na kushirikiana nao kwa wema kwa sababu wao wanajitahidi mno kwenye harakati zao. Isitoshe, wao wanahitaji ilimu zaidi kutoka kwa wale wanaoweza kuwazindua wao miongoni mwa wanavyuoni wa Tawheed na Sunnah. Tunamuomba Mwenyezi Mungu(Subhaanahu wata'aalah) ampe kila mmoja ufahamu wa Dini na Amthibitishe juu ya msimamo wa kisawasawa.

Ama kuhusu swala za ndani ya misikiti yenye makaburi, basi swala hizo hazifai na inakupasa uzirudie zote ulokwisha kuziswali humo (kwenye misikiti hiyo), kwa ushahidi wa maneno ya Mtume(Sallallahu 'alayhi wasallam)aliposema: 'Mwenyezi Mungu Amewalaani Mayahudi na Manaswara kwa kuyafanya makaburi ya mitume yao kuwa ni sehemu za 'Ibaadah' (Usaheeh wake umeafikiwa). Pia kama alivyosema tena (Sallallahu 'alayhi wasallam): 'Kwa hakika wale waliokuwepo kabla yenu walikuwa wakiyafanya makaburi ya mitume yao na watu wema kuwa ni sehemu za 'Ibaadah, kwahivyo musiyafanye makaburi kuwa ni sehemu za kufanya 'Ibaadah, kwa hakika mimi ninawakataza kufanya hivyo.' (Imepokewa na Muslim)

Na Ahaadeeth kuhusu mas-ala haya ni nyingi sana- Na kufuzu ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Tunamuomba Mwenyezi Mungu Amswalie Mtume wetu Muhammad, ahli zake na Maswahaba zake." [Fatwa tarehe 2/11/1414 A.H]

Kuhusiana na maneno ya Sheikh 'Abdul-'Azeez bin Baaz (Rahimahullaah) aliyosema: 'kwahivyo hairuhusiwi kutembea nao isipokuwa kwa yule mwenye ilimu ya kweli ya 'aqeedah saheeh ya Ahlus-Sunnah wal-Jamaa'ah. Katika hali hii, anaweza kuwazindua, kuwapa nasiha na kushirikiana nao kwa wema' Mimi nasema: "Mwenyezi Mungu Amrehemu Sheikh kwani lau kama wangelizikubali nasiha na uongofu kutoka kwa wenye ilimu, basi hakungelikuwa na madhara yoyote katika kutoka nao. Hata hivyo ukweli ni kwamba hawakubali nasiha wala hawauwachi upotofu wao kwa uzito wa utiifu walonao na kujisalimisha kwao kwa Hawaa (mapendelewa ya nafsi) zao. Wangelikubali nasiha za wanavyuoni, basi wangeli-wachilia mbali manhaj yao potofu na kuandama njia ya Ahlut-Tawheed na Sunnah.

Ikiwa hali ndio kama hiyo, basi vivyo hivyo hairuhusiwi kutembea nao kulingana na msimamo wa manhaj ya Salaf as-Saalih, iliyojengwa juu ya Kitaab na Sunnah, kuhadharisha dhidi ya watu wa bid'ah na kuepuka matangamano na ushirikiano nao. Hii ni kwa sababu katika mambo hayo (ya kutembea nao) ni kuongeza idadi yao na kuwasaidia na kuwapa nguvu, katika kuusambaza upotofu wao, na huko ni kuupotoa (kwa jina la) Uislamu na pia kuwapoteza Waislamu na (hatimae) kuwadanganya wao (Jamaa'at ut-Tableegh) na kuwasaidia wao kwenye madhambi na vitendo viovu".

Fatwa ya Imaam Naasir-ud-Deen Al-Albaanee (Endelea)