Jitahadhari na (watu wa) Surooree!
Imetayarishwa Na: Sheikh Muqbil Ibn Haadee Al-Waadi'ee
Imefasiriwa Na: Abu Farida Muhammad A Basawad
Asili: Kitabu cha Tuhfat-ul-Mujeeb 'alaa As'ilat-il-Haadir wal-Ghareeb (uk. 179-185) ambacho ni kitabu kilichokusanya baadhi ya Fataawaa zake.

Bismillaahir Rahmaanir Raheem

"Na linapowafika jambo lolote la amani au la khofu hulitangaza. Na kama wangelilipeleka kwa Mtume na kwa wenye mamlaka kwao, wale wanaopeleleza (wanaojua kupima mambo) miongoni mwao wangalijua (kuwa hilo ni jambo la kutangazwa au si la kutangazwa)." [Soorah An-Nisaa 4:83]

Kwahivyo tunawajibika sisi kurudi kwa Wanavyuoni: "Na hiyo mifano tunawapigia watu; na hawaifahamu ila wajuao." [Soorah Al-'Ankaboot 29:43]

Lakini utakacho ona ni mtu ahifadhi masomo yake mawili au matatu kisha azunguke nayo kwenye misikiti, akichemka na kunguruma (kama beberu). Kisha maswaahib alionao wambandike jina Shaikh-ul-Islaam! Haya jamani hii ndiyo ilimu? Bali, ilimu ni kukaa juu ya jamvi (mkeka) na shida zako ukazipiga ubindo (ili usikilize kutoka kwa Sheikh) - uvumilie kwa kusubiri, shida ya njaa na hali ya ukame. Hebu angalieni hali walizokuwa nazo Maswahaba wa Mtume (Sallallaahu 'alayhi wasallam) na yale waliyoyapitia.

Na wanavyuoni ndiwo wenye kuweka kila jambo mahala pake, kama ilivyosemwa katika aya ilivyotangulia. Na Allaah ('Azza wa jall) Akasema, (kama ilivyofasiriwa): "Kwa yakini katika haya zimo Ishara kwa wenye ujuzi." [Soorah Ar-Room 30:22]

Na Akasema Allaah ('Azza wa jall), (kama ilivyofasiriwa):

"Je! Anayejua yakwamba yaliyoteremshwa kwako kutoka kwa Mola wako ni haki (akayafuata, basi) ni kama aliye kipofu? Wenye akili ndiwo wanaozingatia." [Soorah Ar-Ra'ad 13:19]

Maafa wanayojaribiwa nayo Waislamu ni kutokana na utovu wa ilimu ya Dini yao. Utaona kila anaehifadhi baadhi ya aya chache na ahaadeeth kisha akaanza kuzichambua, haswa ikiwa atakuwa na ubingwa wa lugha, watu watasema: "Huyu ni Sheikh."

Alhamdulillaah, ukweli wa mambo ukadhihiri, kama ilivyosemwa:

"Utakapomsikia bingwa wa lugha akizungumza, usijisalimishe kwake
Njia hii bandia (ya uzungumzaji) ni kitu cha kubuni
Ridhika kwa kuchukuwa ilimu na maarifa, na
Ubingwa wake wa lugha utafikia ukingoni bila ya ugomvi kuwepo."


Allaah ('Azza wa jall) Akasema Alipotusimulia kuhusu kisa cha Qaaroon: "Basi (Qaaroon) akawatokea watu wake katika pambo lake. Wakasema wale wanaotaka maisha ya dunia: 'Laiti tungalipata kama aliyopewa Qaaroon; hakika yeye ni mwenye bahati kubwa.' Na wakasema wale waliopewa ilimu: 'Ole wenu! Malipo ya Mwenyezi Mungu ni mazuri kwa yule anayeamini na kufanya vitendo vizuri (kuliko aliyonayo huyu Qaaroon) wala hawatapewa hayo isipokuwa wafanyao subira.' Basi tukamdidimiza yeye (Qaaroon) na nyumba yake ardhini; wala hapakuwa na kundi lolote la kumsaidia kinyume na Mwenyezi Mungu, wala hakuwa miongoni mwa walioweza kujisaidia. Na wakawa wanasema wale waliotamani cheo chake jana: 'E-e-e- (kweli) Mwenyezi Mungu Humzidishia riziki amtakaye miongoni mwa waja wake (na haliyakuwa mbaya, hampendi), Na hudhikisha (riziki ya anayemtaka); Asingetufanyia hisani Mwenyezi Mungu bila shaka Angetudidimiza (kama Alivyomdidimiza kwani sisi tuliitamani hali yake) O! kweli hawafuzu makafiri." [Soorah Al-Qasas 28:79-82]

Basi ni wajibu wetu kurudi kwa Wanavyuoni na kusoma, kama ambavyo Jibreel ('Alayhis Salaam) alivyokwenda kwa Mtume (Sallallaahu 'alayhi wasallam) ili awafundishe Maswahaba jinsi ya kuuliza masuali.

Na sitosahau yale aliyoyasema 'Abdul-Qaadir Ash-Shaybaanee, kijana mjinga: "Tutawapeleka baadhi ya ndugu zetu kwa Abee 'Abdir-Rahmaan (yaani Sheikh Muqbil) ili nao wapate mikupuo (ya ilimu) kwa kiasi cha miezi miwili, kisha tuwapeleke kwenye baadhi ya vyuo ili tuwapokonye viwanja (watu wa) Ikhwaan al-Muslimeen." Mimi nikasema: "Kwa muda wa miezi miwili pana uwezekano gani wa kuzalisha walinganizi katika Da'wah?"

Ikiwa watu wajinga ndiwo wenye kuyasimamia mapote ya walinganizi wa Da'wah, basi mimi nawapa bishara ya mauti ya mapote hayo. Kwahivyo tunawajibika sisi kujiambatanisha na Wanavyuoni na kutafuta ilimu kutoka kwao, kama vile ambavyo walivyofanya Wanavyuoni wetu wa kale. Salmaan Al-Faarisee alikaa na kutafuta ilimu kwa Mwanachuoni wa kwanza aliyekutana nae mpaka (yule mwanachuoni) akafikwa na mauti, na kisha wa pili na wa tatu hadi alipomfikia Mtume Muhammad (Sallallaahu 'alayhi wasallam) na akamfuata. Na hivi ndivyo walivyokuwa wanafunzi wa Mu'aadh (Radhiallaahu 'anhu). Kabla ya kufa kwake, walimuuliza: "Sisi twende wapi (kutafuta ilimu baada ya kuondoka kwako)?" Akawaambia: "Kwa 'Abdullaah Ibn Mas'ood."

Soma Ukurasa wa Mwisho