Jitahadhari na (watu wa) Surooree!
Imetayarishwa Na: Sheikh Muqbil Ibn Haadee Al-Waadi'ee
Imefasiriwa Na: Abu Farida Muhammad A Basawad
Asili: Kitabu cha Tuhfat-ul-Mujeeb 'alaa As'ilat-il-Haadir wal-Ghareeb (uk. 179-185) ambacho ni kitabu kilichokusanya baadhi ya Fataawaa zake.

Bismillaahir Rahmaanir Raheem

Na itokeapo mmoja miongoni mwa ndugu zetu wakiwakazia kamba (watu wa) Hizbee ili wakatafute ilimu kwa kuwaambia: "Wako miongoni mwenu wanaopenda dunia, na wako miongoni mwenu wanaopenda Akhera." [Soorah Aali 'Imraan 3:152] Hapo utamsikia (mtu wa Hizbee) akijibu:

"Allaah (Subhaanahu wata'aalah) Aliiteremsha aya hii kuwahusu Maswahaba" - kwa maana yakwamba, wao wanakiri (wanakubali) yakuwa hawana uvumilivu katika kutafuta ilimu na kuistahamili njaa. Badala yake wao hupendelea kuishi karibu na watu kwenye majumba na magari na kupenda mambo ya anasa za ki-dunia.

Kisha utawasikia wao wakisema: "Nyinyi kazi yenu ni kuvishambulia vyama vyote." Haya ni nani aliyewaambia yakuwa sisi twavishambulia vyama? Naam, sisi twavishambulia baadhi ya vyama vyenye ta'assub , wenye ushupavu wa Walaa (utiifu), unyang'anyi na ufujaji wa pesa. Hizi ndizo aina za mapote tunayo yalaumu na kuwaonya watu wajitahadhari nao.

Basi jueni na kutanabahi! Yakwamba hii ni Da'wah (mwito) ambayo iliyo juu ya msingi wa udanganyifu na ulaghai, lakini ukweli wa mambo utadhihiri hivi karibuni. Kwani Da'wah ya 'Alee Ibn Al-Fadl ilidhihiri yenyewe na vilevile ukweli wa Da'wah ya Mu'tazilah, (watu wa) Shia'ah na (watu wa) Soofee wakajidhihirisha wenyewe. Na watakaowafichua na kuzidhihirisha njama hizi, kwa uwezo wake Allaah (Subhaanahu wata'aalah), ni Ahlus-Sunnah.

Walhamdulillaah! Ahlus-Sunnah peke yake ndiwo wenye kuyafuatilia na kuleta marekebisho katika Ummah wa Kiislamu. Alisema Mtume (Sallallaahu 'alayhi wasallam): "Hapatokosekana kuwepo pote miongoni mwa Ummah wangu ambalo linalojidhihirisha juu ya haki. Wale wenye kuwapiga wao vita hawatoweza kuwadhuru kwa chochote mpaka itakapopita amri ya Allaah (yaani: Ahadi) haliyakuwa wao wapo juu ya msimamo (hali hiyo)."

Kwahivyo Sheikh Rabee' Ibn Haadee (Hafidhahullaah), akiwa katika nchi za Haramayn na Najd, anawafichua (watu wa) Hizbee na kuzichambua itikadi walizo nazo. Na vilevile Sheikh Abul-Hasan aliyeko Ma'rib na Sheikh Muhammad Ibn 'Abdil-Wahhaab aliye Hudaydah na Sheikh Muhammad Al-Imaam aliye Ma'bar na Sheikh Qaasim na ndugu Muhammad As-Somalee aliye Jaami'-ul-Khair huko San'aa.

Basi mimi natoa nasiha kwa ndugu zangu, kwa sababu wengi wao WALHAMDULILLAAH ni wenye kusikiya, warudi katika Qur'aan na Sunnah na walinganie watu juu ya hayo, na wasijipotezee maisha yao kwa kuwasifu Mashekhe fulani na fulani. Na lau ikibidi kujitenga na Mashekhe hao, wakaanza kusema: "Jitahadhari nae, huyo ni katika Jamaa'at At-Takfeer" au "Huyo ni kibaraka cha Serikali." Haya ni maneno ya yule asiyemcha Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wata'aalah).

Kumbukumbu

[1] Tanbeeh ya mfasiri: Neno hili ni wingi wa neno la Kiarabu "miskeen", lenye maana ya muhitaji. Katika kifungu hichi cha haya maneno imehusu mtu fulani aliye mjinga wa ukosefu wa ilimu, kwahivyo ndio akawa muhitaji (wa hiyo ilimu).