Suluhisho La Matatizo Ya Umma Huu
Na: Imaam Muhammad Naasir ud-Deen al-Albaanee
Asili: Manhaj ya Salafi
Imefasiriwa Na: Abufarida Muhammad A. Basawad

Bismillaahir Rahmaanir Raheem

Ni kutokamana na mahitaji mawili, yaliyo muhimu sana, yanayotupasa kuyaunganisha:

  1. Mwito wa katika Qur'an na sunna.
  2. Kuwepo juu ya msimamo walokuwa nao watangulizi wetu wema (As-salaf-us-saalih),kwa kuyatekeleza yale yalokwisha tajwa hapo mbeleni kwenye baadhi ya aya na hadith.
Kama vile alivyotaja Mwenyezi Mungu "njia ya waumini" na pia Mtume (S.A.W) na maswahaba zake kutuashiria yakwamba kuifahamu Qur'an na Sunnah kunapaswa kutegemezwa juu ya msimamo walokuwa nao watangulizi wetu wa kwanza (Salaf), kuanzia maswahaba na wale walowafuata wao kwa wema.
Na hapa kuna suala muhimu sana , ambalo mapote mengi ya ki-islamu na vyama wamelipuuza. Suala lenyewe ni: "Ni njia gani hiyo inayotuelekeza kwenye kuipata ilimu walojitigemeza nayo maswahaba wa Mtume (S.A.W) kulingana na msimamo thabiti wa sunna hii?"
Jawabu ni kwamba :Hakuna njia ya kuifahamu isipokuwa ni kurudi kwenye utaalamu wa hadith, utaalamu wa Al-Jarh wat-ta'dil (utaalamu wa kuwabainisha wapokezi iwapo ni wenye kutegemeka au la), na utekelezaji wa kanuni zake na masharti yake. Ili wanavyuoni waweze kuzitambua riwaya zilizo sahih kumuhusu mtume (S.A.W) kutokamana na zisizo sahih.

Kwa mujibu wa kumalizia jawabu hili-tunasema -kwa maneno ya wazi- kwa waislamu wenye hamu kubwa za kuregesha utukufu, ta'adhima,na mamlaka, katika Uislamu, yakwamba ni lazima muzingatie mambo mawili:
Amma kuhusu jambo la kwanza, basi ni lazima ufanye muungano na uregeshe ndani ya fikra za waislamu, Dini ya waislamu iliyotahirika kutokamana na yote yaliyoingizwa ndani yake; ambayo hayakuwa ni sehemu yake siku ambayo Mwenyezi Mungu (Swt) Mtukufu, Mwenye Nguvu alipoteremsha maneno Yake Akisema:
"Leo nimekukamilishieni dini yenu, na kukutimizieni neema Yangu, na nimekupendeleeni Uislamu Uwe dini yenu."9

Na kuregea kwenye hali hii, leo- kama ilivyokuwa kwenye nyakati za mwanzo -kunahitaji juhudi kubwa na hima kwa upande wa wanavyuoni kwenye sehemu tafauti za ulimwengu.
Jambo la pili ni kwamba: kuwa na msimamo na kupambana kwa bidii (kuurekebisha umma) ni lazima kutimizwe na hii ilimu iliyotakata. Kwahivyo, siku ambayo wailslamu watakaporudi kwenye kuifahamu dini yao, kama walivyoifahamu maswahaba wa mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W), na kisha wao wakashughulika kama inavyowajibika kulingana na Uislamu ulotakata, ulio juu ya misingi ya vitendo vizuri katika kila jinsi ya kimaisha, basi ni katika siku hiyo ambapo wislamu watakapo sherehekea ushindi wa Mwenyezi Mungu.
Haya ndiyo niliyoweza kuyasema katika huu ulinganizi ulokusanywa pamoja kwa haraka. Namuomba Mwenyezi Mungu Atujaalie sisi na Waislamu wote tuwe na fahamu njema ya uislamu ulo juu ya msingi wa muangaza wa kitabu chake, Sunna zilizo Sahih za Mtume Wake (S.A.W) na yale ambayo watangulizi wetu wema (As-Salaf-us-Saalih) waliojitegemeza nayo. Na tunamuomba Atuwezeshe kuyatekeleza hayo. Kwa hakika Yeye ndiye Anaesikiya na Anaejibu.


Foot notes:
  1. As-Sahiha # 11
  2. Surat Al-Maidah 5:3
  3. Surat Al-an-am 6:153
  4. Hadith sahihi kama ilivyopewa daraja katika dhilaal-ul-jannah fee takhreej-is-sunna(16-17).
  5. Surat- An-Nisaa 4:115
  6. As-Sahiha # 203
  7. Sahih Al-jaami' #1641
  8. Sahih al-Bukhari
  9. Surat Al-Maidah 5:3