
Ikishafahamika kwamba mwenye kuacha swala ni kafiri basi ifahamike kuwa zitafungamana kwa mtu huyo hukumu za murtaddi (mtu alietoka katika uislamu) wala hakuna katika nassi za Qur-ani au za Hadeeth zinazo onyesha kwamba mtu asie swali ni muislam au ataingia peponi au atapona na moto.
Miongoni mwa hukumu zitakazo fungamana na mtu asie swali ni hizi:
1- Sihalali kuozeshwa (mwanamke wa kiislamu) na akiozeshwa na hali haswali ndowa haitaswihi na huyo mke si halali kwake. Mwenyezi Mungu anasema: {Mkiwajuwa (hao wanawake) kuwa ni waislamu basi msiwarudishe kwa makafiri hao (wanawake) si halali kwao wala hao (wanaume makafiri) si halali kwa hao wanawake wakiislamu} (Surat Mumtahinah Aya ya 10).
2- Akiacha kuswali baada ya ndowa basi ndowa hiyo itafasihika (itavunjika), na huyo mwanamke hatokuwa halali kwake kwa ushahidi wa aya ilyotajwa hapo juu.
3- Mtu asieswali akichinja ni haramu kula alicho kichinja, tofauti na kilicho chinjwa na myahudi au mnaswara ni halali kukila, basi huwa Mwenyezi Mungu Atulinde, kichinjo (cha asieswali) ni kiovu kuliko kichinjo cha myahudi au mnaswara.
4- Si halali kwa taarikuswalat kuingia Makkah au kuvuka mipaka yake, Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wata'aalah) anasema katika Qur'aan: {Enyi mlio amini hakika makafiri ni najisi kwa hiyo wasiukurubie Msikiti Mtukufu baada ya mwaka wao huu} (Surat Tawbah Aya ya 28).
5- Akifa mmoja kati ya jamaa zake (mtu asieswali) hana haki ya mirathi, kwa mfano akifa mtu akamuacha mtoto wake taarikuswalat na mtoto wa ami yaka (anaeswali) basi atakaerithi ni mtoto wa ami yake. Ushahidi ni maneno ya Mtume (Sallallahu 'alayhi wasallam) katika hadeeth ya Usaamah: Muislamu hamrithi kafiri wala kafiri hamrithi muislamu.
6- Akifa (taarikuswalat) haoshwi wala hakafiniwi wala haswaliwi wala hazikwi pamoja na waisilamu, basi tumfanyie nini? Bali mtu huyo atatolewa apelekwe jangwani achimbiwe shimo afukiwe na nguo zake kwa sababu mtu huyo hana heshima yoyote katika Uisilamu kwa hiyo mtu atakaekuwa na maiti na anajuwa kwamba maiti huyo alikuwa haswali asimpeleke kwa waislamu ili wamswalie.
7- Mtu asie swali atafufuliwa siku ya kiama pamoja na Fir-aun na Haamaan na Qaaruun na Ubayy bin Khalaf, viongozi wa ukafiri (Mwenyezi Mungu atulinde na ukafiri) wala hatoingia peponi wala sihalali kwa jamaa zake kumuombea dua za rehma na msamaha kwa sababu ni kafiri hastahiki kuombewa dua Mwenyezi Mungu anasema: {Hairuhusiwi kwa Mtume na wale walioamini kuwaombea dua makafiri wajapokuwa ndugu zao wa karibu, baada ya kuwabainikia hao ni watu wa motoni} (Surat Tawbah Aya ya 113)
Haya mambo ndugu zangu ni khatari sana. Kwa bahati mbaya kuna baadi ya watu hudharau amri hii, na hukaa nyumbani na wasio swali na hili jambo halifai, hii ndiyo hukumu ya taarikusalat awe ni mume au mke.
Ewe ndugu usie swali au unae fanya mchezo katika swala, iwahi sehemu iliyobaki katika umri wako kwa amali njema, hujuwi umebakisha siku ngapi miezi michache au siku chache au saa chache kumbuka kauli ya Allah (Subhaanahu wata'aalah): {Hakika atakae mjia Mola wake na hali amefanya madhambi makubwa basi stahiki yake ni moto wa jahannam hatokufa humo wala hatokuwa hai} (Surat Twaaha Aya 74), pia kumbuka kauli ya Allah (Subhaanahu wata'aalah): {Ama mtu atakae pindukia mipaka katika maasi Na akapendelea maisha ya Dunia kuliko Akhera Basi moto wa jahannam ndio makaazi yake} (Surat Naziat Aya 37 39).
Sheikh Muhammad bin Saaleh bin Uthaimin (Allah amrehemu)
Ndugu Muislamu baada ya kuyasoma haya na ampe mwenziwe (Mwenye kulekeza njia ya kheri ni kama alietenda).
|