
Suali:
Nini hukmu ya wanawake wanao sali msikitini ambapo hawamwoni Imaam wala wanaume wanao sali nyuma ya Imaam, bali wanamsikia sauti yake pekee?
Jawabu:
Sifa zote ni zenye kumthubutukia Allah.
Yaruhusiwa kwa wanawake, hata wanaume, kusali na jamaa msikitini hata kama hawamwoni Imaam au wanaume wanao sali nyuma ya Imaam, iwapo wataweza kumfuata imaam. Ikiwa sauti itafika mahala wanawake wanaposali katika sehemu yao ya msikiti na wanaweza kufuata kisomo cha Imaam, basi inasihi kwao kusali nyuma ya imaam huyo, kwa sababu yote hayo ni mahala moja, na yawezekana kumfuata imaam kwa kusikia sauti yake kutoka kwa kipaza sauti (loud speakers) au kwa kusikia sauti yake moja kwa moja, au kupitia kwa mtu anaye rudia takbeer ya imaam. Sio neno kama hawamwoni Imaam au wanaume nyuma yake. Bali baadhi ya maulamaa wanao rai kuwa ni sharti wamwone imaam au wanao sali nyuma yake kwa watu wanao sali nje ya msikiti.
Ma fuqahaa (wanavyuoni) wamesema kuwa mtu anayesali nje ya msikiti sala yake inasihi tu iwapo anaweza kumwona imaam au watu wanao sali nyuma yake. Lakini rai ilio sawa kulingana na mimi ni kuwa haisihi kwa mtu kumfuata imaam ikiwa anasali nje ya msikiti hata kama anamwona imaam au wanaosali nyuma yake, iwapo kunao nafasi ndani ya msikiti anapoweza kusali. Hii ni kwa sababu makusudio ya kusali kwa jama'a ni kuwaleta watu na amali zao pamoja mahala moja. Lakini iwapo msikiti umejaa na wale wanao sali nje ya msikiti wanamfuata imaam, basi rai ilio sahih ni kuwa inaruhusiwa kwa wao kumfuata imaam, iwapo wanamwona au laa, maadamu safu zao zinaendelea.
Majmoo' Fataawa al-Shaykh Ibn ‘Uthaymeen (15/213)
|